Kuanzishwa Kwako Uzazi na Dawa

Questions or concerns about your induction?

Asante kwa kuchagua Norton Women’s Care kwa huduma yako ya kujifungua.

Umepangiwa kuanzishwa uzazi kwa dawa katika tarehe isiyo thabiti katika Hospitali ya Norton Women’s & Children’s Hospital.

Mfanyikazi kutoka idara ya uzazi na kujifungua atakupigia katika siku yako ya kuanzishwa uzazi ili kukujulisha iwapo kuna kitanda lenye nafasi. Hakikisha kwamba taarifa yako ya kimawasiliano katika akaunti yako ya Norton MyChart  iko sawasawa na kwamba umetupatia idhini ya kuwasiliana nawe.

Kujifungua na kupata mtoto ni muda wa furaha na wasiwasi! Kuna mambo mengi ya kufikiria na kujitayarishia, haswa kabla ya kujifungua uliyopangiwa awali.

Kwa Uzazi wa Kuanzishwa na Dawa wa Hiari

  • Kuanzishwa uzazi na dawa wa hiari hufanyika wakati wewe na daktari wako wa uzazi mtakapoamua kuanzisha mchakato wa kujifungua kwa sababu zisizo za kimatibabu.
  • Kuanzishwa uzazi na dawa wa hiari haiwezi kufanywa kabla ya wiki yako ya 39 ya mimba.
  • Kuanzishwa uzazi na dawa wa hiari unaweza kusababisha:
    • Kuongezeka kwa muda wa kujifungua kwako na kukaa hospitalini.
    • Kuongezeka kwa dawa ya maumivu na/au dawa ya kuua ganzi.
    • Kupunguka kwa uwezo wako wa kutembea tembea katika chumba cha kujifungua.
    • Kuongezeka kwa uwezekano wa kujifungua kupitia upasuaji.
  • Kwa bahati mbaya, watoto wengi huwa hawafiki katika muda iliyopangwa, kwa hivyo upatikanaji wa nafasi katika vitengo vya kujifungua na uzazi hazijulikani kila mara. Tarehe uliyopangiwa kuanzishwa kujifungua ni tarehe isiyo thabiti.
  • Wahudumu wa uzazi na kujifungua huwahudumia wagonjwa kulingana na kipaumbele ya kiafya. Hii inaweza kusababisha kuahirishwa kwa kuanzishwa uzazi na kujifungua kwako.

Kujitayarisha Kwa Kujifungua Kwako Uliyopangiwa

  • Usinyoe kutoka kiuno hadi miguu, ikiwamo mavuzi, kuanzia siku tatu kabla ya tarehe isiyo thabiti uliyopangiwa kuanzishwa uzazi. Hii itasaidia kuzuia uwepo wa maambukizi.
  • Kula chakula hafifu kabla ya kuja hospitalini. Vyakula ambavyo vina protein na aina za kabohaidreti za kiafya, kama mayai na tosti ya unga kamilifu, au yogurt iliyo na matunda.
  • Iwapo mtoa huduma wako wa bima atahitaji idhini ya awali, basi ni lazima uwaarifu kuhusu uzazi wako wa kuanzishwa uliyopangiwa haraka iwezekanavyo ili kuhakikisha utapokea fidia kamili ya bima yako.
  • Iwapo unapangia kuzibwa mishipa ya uzazi wakati wa kujifungua, hakikisha umeleta karatasi ya idhini uliyopatiwa hapo awali.
  • Iwapo utahitaji kupanga upya au kutupilia mbali miadi yako ya kuanzishwa uzazi na dawa, pigia ofisi ya daktari wako leo kabla ya saa 3 jioni siku moja kabla ya tarehe isiyo thabiti uliyopangiwa kuanzishwa uzazi.

Iwapo utakumbana na hali ya kidharura kabla ya tarehe ya miaadi yako, nenda kwa idara ya hali ya dharura ama pigia 911.

Pigia Hospitali ya Norton Women’s & Children’s Hospital kupitia (502) 893-1270 ikiwa una maswali yeyote au wasiwasi kuhusu kuanzishwa uzazi wako.

Kuegesha Gari na Maelekezo

Muda wa kuja hospitali ukifika, ingia Hospitali ya Norton Healthcare – St. Matthews kupitia Kiingilio cha (Entrance) 4. Egesha gari katika eneo la maegesho la Norton Medical Plaza 3 – St. Matthews katika 4123 Dutchmans Lane au katika eneo la maegesho kando ya mlango wa Norton Medical Plaza 3 – St. Matthews.

Kuegeshewa gari na wahudumu au valet wa bure unapatikana kutoka Jumatatu hadi Ijumaa, kutoka 6 asubuhi hadi 6 jioni katika mlango wa Norton Medical Plaza 3 – St. Matthews na katika mlango mkuu wa hospitali. Utakapoingia Norton Medical Plaza 3 – St. Matthews, panda lifti yenye rangi ya dhahabu hadi ghorofa ya pili. Nenda hadi ufike kwa meza ya kulazwa kwa uzazi na kujifungua.

Tuna furaha kuwa na wewe katika muda huu wa kipekee katika maisha yako! Tunatarajia kukuona siku karibu.

What to Expect from Norton Women’s Care

More mothers in Louisville and Southern Indiana choose to deliver their babies at Norton Hospital or Norton Women’s & Children’s Hospital than with any other hospital system in the area.

We deliver more than 8,000 babies a year. We’re close to you with more than 90 providers at more than 25 locations around Louisville and Southern Indiana. Choosing Norton Women’s Care gives you many options for how delivery day could go — all with the confidence of knowing that our obstetrics and pediatric specialists are there to help. With Norton Women’s Care, you’ll find:

  • The birth experience you want: You can choose natural childbirth, a midwife, labor tub, nitrous oxide and other birthing options. We’ll recommend a C-section (cesarean section) or induced labor only if it’s medically necessary.
  • Preparation: Our specialists offer the support you need, including free Lamaze and other childbirth classesnew parent classesbreastfeeding supportchild safety classes and more.
  • Confidence and quality in care: Norton Women’s Care has been recognized as High Performing — the highest rating available — for maternity care with fewer complications and C-sections, plus breastfeeding support and other benefits.
  • We offer the highest-level (Level IV) neonatal intensive care unit (NICU) in Louisville and Southern Indiana at Norton Children’s Hospital, and a sophisticated Level III NICU at Norton Women’s & Children’s Hospital.
  • Around-the-clock OB/GYN care is available at Norton Hospital and Norton Women’s & Children’s Hospital emergency departments.
  • Our board-certified maternal-fetal medicine specialists  can help guide you through a high-risk pregnancy, from treating preexisting diabetes in the pregnant patient to a fetal echocardiogram to diagnose a congenital heart condition before a baby is born.
  • Medicare, Medicaid and most major commercial insurance plans are accepted.
  • Convenient access to your medical record: Communicate with your health care provider, get lab results, renew prescriptions and more through your free Norton MyChart account.

Related Stories

Norton Clark Hospital recognized for excellence in infant, maternal health
First in area: Wendy Novak Diabetes Institute Perinatal Program established for specialized care
Norton Clark Hospital receives newborn training mannequin
New rooms give patients options for childbirth